MWASENDA DEVELOPMENT INTERVENTION (MDI - NGO)

CHAKULA CHA AKILI (MENTAL FOOD)

LAWAMA, HUKUMU NA MAJUTO USIYOSTAHILI.

Tuwende tukaangalie LAWAMA NA MAJUTO USIYOSTAHILI kama moja ya vitu usivyopaswa kuvifanya. Shaka hakuna kuwa utakuwa unakumbuka vyema yale makundi mawili kama umeyasahau rejea kusoma somo lililopita; Mwishoni mwa somo tuliongelea lawama na hukumu zinakubaliwa katika kundi la pili ambalo tuliona kuwa  linahusika na kuipuuza sauti ya ndani (inner voice) ambapo mwili hutawaliwa na nguvu ya milango ya fahamu, ni hapa ambapo tunapata neno tamaa na hapa huhusika na masuala ya hisia kama mapenzi.

Katika kundi hilo la pili lawama, hukumu na majuto utakayoyapata baada ya matokeo kuja hasi hapo unastahili, kwa kukosa nidhamu juu ya ubinadamu wako na kuziheshimu tamaa, lakini hapa tutakuja kupaangalia zaidi katika masomo yatakayohusu HISIA (EMOTIONS) maana hatutaacha nyanja yoyote inayogusa maisha, na pia kukubaliwa kwa lawama, hukumu na majuto haitakuwa sababu ya kushindwa maisha. Hivyo hali hii haitakubaliwa kudumu hata ikitokea ili kuruhusu shughuli zingine ndani ya ubongo ziendelee na maisha yaendelee pia.

Na pia kama uliongozwa na sauti ya ndani kufanya kitendo chochote cha kihisia na ukapata matokeo hasi hutapaswa kujilaumu juu ya hilo ila utapaswa kutoka kwenye hilo, kwanini usijilaumu? Maelezo yake yataendana na namna nitakavyoeleza katika kundi la pili twende tukaliangalie.

Kundi la pili lile  ambalo binadamu anajengwa katika msingi wa neno KAWAIDA ambapo hapa panahusisha shughuli zinazomuingizia kipato, hapa pia ataruhusiwa kujilaumu endapo amepata matokeo hasi ya shughuli yoyote kwasababu aliufata msingi KAWAIDA na kuipuuza sauti ya ndani. Vivyo hivyo hali hiyo haitatakiwa kudumu. Pale inakuwa imetokea ili shughuli zingine za ubongo ziendelee na maisha yaendelee.

Lakini vipi pale endapo matokeo  yatakuja hasi na wakati uliisikiliza sauti ya ndani?  Usijilaumu wala kujutia wala kujihukumu kwanini. Hapa tukajifunze jambo la muhimu sana ndipo msingi wa somo hili unaposimama. Kuna vitu viwili vinavyotokea katika shughuli yoyote uwe makini hapa, vitu vyenyewe ni dhamira au nia NA matokeo, hivi ni vitu viwili tofauti ambavyo ni lazima vitatokea katika shughuli yoyote ile. Dhamira siku zote huwa na upande mmoja yaani huwa CHANYA lakini matokeao huwa na pande mbili HASI NA CHANYA. Hivyo lazima matokeo yataegemea upande mmoja, tutajikita zaidi kwenye upande HASI maana huku ndiko kwenye lawama, majuto na hukumu juu yako mwenyewe.

Hupaswi kujilaumu, kujihukumu wala kujutia kwa matokeo hasi kwa sababu   binadamu yeyote mwenye akili timamu ni lazima atakuwa na DHAMIRA njema kabla ya kutekeleza shughuli yoyote. Hivyo usijilaumu kwasababu ya matokeo ndiyo maana kama wewe ni mkulima uliwahi kila siku saa kumi na moja kwenda shamba, ukashinda huko mpaka jua lilipozama, pengine ukashinda hata na njaa. Kama wewe ni mfanyabiashara pengine ulitembea umbali mrefu kufuata bidhaa zako pengine ulitukanwa hata na wateja wako lakini bado ulifanya kwa moyo mmoja.  Ulifanya hayo yote kwa sababu ya DHAMIRA iliyokuwa njema lakini mavuno yanapokosekana shambani au hasara yoyote inapotekea katika biashara siyo sababu ya kujilaumu wala kujihukumu, kwasababu kwa kila shughuli  unayopanga kuianza kabla ya kuifanya hauwezi ukapanga kuja kupata matokeo hasi.

Hivyo dhamira itabaki lengo kuu na matokeo yatabaki kama matokeo. Hivyo  matokeo hasi yanakuja ili kuboresha ufahamu wako. Hatuna neno KUSHINDWA pale matokeo yanapokuja hasi ila tuna maneno haya “Njia ambazo hazijaleta matokeo sahihi kulingana na dhamira” Hivyo inakuhitaji ubadili njia na kubadili njia kunawezekana tu endapo akili yako haitakuwa na hatia juu yako. Hivyo yakupasa kuupa ubongo wako nguvu ya kusukuma akili nyingi ili kuleta njia zingine bora.

Ubongo  SUPERIOR unakuwa bize kutafuta njia bora wakati ubongo wa wanajamii unakuwa bize kwenye kujutia na kujihukumu. Homework kwako mwanajamii … “unafikiri ni nani ataendelea kusonga mbele kati ya hawa watu wawili; anayetafuta njia au  anayejihukumu?

Kuna huyu jamaa anaitwa THOMAS EDSON mgunduzi wa bulbu anasema, katika jaribio lake la ugunduzi wa bulbu SIKUFELI MARA elfu kumi ila nilitumia NJIA elfu kumi ambazo hazikunipa majibu sahihi katika ugunduzi wa bulbu. Kataa neno kufeli,  litoe akilini mwako – songa mbele.

TUONANE SOMO LA NANE …

Leave a Reply