MWASENDA DEVELOPMENT INTERVENTION (MDI - NGO)

ELIMU TUNAYOITOA TANZANIA NI ELIMU YA KUKARIRISHANA NA INAUA VIPAJI VYA WATANZANIA.

ELIMU TUNAYOITOA TANZANIA NI ELIMU YA KUKARIRISHANA NA INAUA VIPAJI VYA WATANZANIA.

Kuna mambo mawili nitayazungumza leo kuhusu Elimu yetu. Moja ni lugha tunayoitumia kifufundishia mashuleni na cha pili ni tunachofundishwa (content).

  1. #LUGHA

Tukianza na hili la kwanza nitawaelezeni kuhusiana na kitu kinachoitwa “Feral Child”

#Feral child ni aina ya watoto wanaokuwa au kukuzwa bila kupata malezi ya Binadamu mwenzao. Kwa maana nyingine tunasema ni watoto wa binadamu waliokuzwa na kulelewa na jamii nyingine za wanyama kama vile jamii ya Sokwe, Mbwa, Mbuzi nk.

Ipo mifano mingi ya watoto kama hawa duniani, hii hapa ni mifano michache tu:-

1.Saturday Mthiyane alipatikana mwaka 1987 huko Kwa Zulu Natal alikuwa kwenye Kundi la Sokwe na alikuwa tayari ameshajifunza tabia zote za Sokwe na alikuwa hawezi kuongea chochote.

2.Baby Hospital (1984) Huko Sierra Leone Wamisionari walimwokoa, alikwa tayari kashajifunza tabia zote za Sokwe na alikuwa hajui kuongea chochote.

3.Oxana Malaya, (1990s)Ukraine, huyu alitelekezwa na wazazi wake huko Ukrain kutokana na ulevi alikuwa akiishi na Mbwa alipokutwa alikuwa tayari ameshajifunza kubweka kama mbwa. Madaktari walimhudumia walidai kuwa alizaliwa akiwa na afya njema kabisa lakini alipookolewa alikuwa tayari anatabia zote za Mbwa.

4.Danielle Crockett, U.S.A aliokolewa na vyombo vya Usalama mtoto huyu kwa kuwa wazazi wake walikuwa wamemtelekeza ndani. Walikuwa wakimfungia ndani kwa hiyo alipata Ulemavu wa viungo na Kushindwa kuongea kwa kuwa hakupata Interactions na binadamu wenzake.

 

NAMAANISHA NINi?

Binadamu hujifunza tabia ikiwemo Lugha kutokana na Mazingira aliyopo. Kama watoto hawa wakati wanazaliwa wangelitunzwa na binadamu basi wangeliweza kuongea na kuwa na tabia za Binadamu.

Nadharia hii nimependa kuitumia siku ya leo ili kuihusianisha na elimu yetu tunayoipata. Leo nitaongelea kipengele kimoja tu cha Lugha.

 

Kwa WATANZANIA walio wengi Lugha yao ya Kwanza kujifunza na wanayoijua kwa ufasaha zaidi ni Lugha za makabila yao.

Mfano Mimi nilizaliwa kule Kagera – Bukoba (Kiziba) na kukulia huko hivyo nilijifunza Kihaya  cha Kiziba  tu na nilikuwa nikimsikia Mnyambo  akiongea siwezi kumjibu au Muyoza  na Muhamba. Niliamini kabisa kwamba wanakosea kuongea – hii ilikuwa wakati wa utoto wangu. Kwenye umri huo nilijifunza kutengeneza vikapu (entukulu), niliweza kuijua hela kwa kuwa vikapu vilikuwa na wateja wengi sana. Nilijifunza kufuga kuku, wa kienyeji. Shuleni (Shule ya Msingi Kikono) nilijifunza mambo mengi ila moja kuu ambalo watoto wetu hawafundishwi ni Sayansi kimu. Kwenye somo hilo tulijifunza mambo mengi sana kwa vitendo, ilikuwa kika siku ya Alhamisi wanafunzi wote tulienda na vifaa kwa ajili ya kujifunza kwa vitendo. Tulijifunza kupika aina tofauti tofauti za vyakula.

Nilipofanikiwa kuingia shule ya upili (Kahororo Secondary), ndo hapo nikachanganyikana na watu wengine toka sehemu mbalimbali.

Naanza la kwanza dhana zote darasani nafundishwa kwa Kiswahili baada ya muda wanaongezea hapo na Kiingereza.

Yaani ipo Kisayansi kuwa Lugha ya kwanza utakayojifunza utakuwa na uelewa nayo mkubwa zaidi kuliko lugha ya pili kujifunza na ya tatu. Kuna baadhi ya makabila wanajua lugha yao hiyo ya kikabila tu. Na Lugha utakayojifunza ukiwa bado na Umri Mdogo unakuwa na uwezo mkubwa sana wa kuimudu kuliko Lugha zozote zile utakazokuja kujifunza baadaye.

Kiswahili ni Lugha yetu ya pili kujifunza, hii tunaimudu vizuri sana kwa kuwa hata kwenye familia zetu tunaiongea. Kiingereza hii ni lugha ya tatu kujifunza kwa hapa kwetu Tanzania kwa waliowengi.

 

SHULENI

Kwa Tanzania Lugha inayotumika kufundishia na kujifunzia ni Mbili tu yaani Kiswahili na Kiingereza. Kiswahili tunakitumia kwa shule za msingi na kiingereza tunakitumia kuanzia sekondari hadi Chuo kikuu.

Nchini Kenya na Uganda lugha ya kufundishia ni Kiingereza isipokuwa kwa baadhi ya masomo.Nchi ya Rwanda ilibadili lugha yake ya kufundishia kutoka Kifaransa hadi Kiingereza.

Nchi nyingi za Ulaya na Amerika zinztumiz Lugha zao kufundishia na mambo yanakuwa marahisi sana. China wameamua kukomaa na kichina chao huko Korea na Kwingineko.

Kuanzia darasa la awali mpaka darasa la saba mtu anasoma kwa Kiswahili miaka yote 8 Halafu miaka 9+ iliyobakia unamwambia atumie Kiingereza. Mtu huyu unamfundisha miezi mitatu English Course halafu unaanza kumfundisha mada na nadharia mbalimbali huu ni utani tunafanya kabisa.

Wahitimu wengi wanamaliza wanaitwa kwenye interview wanashindwa kujieleza na hawa ni wahitimu wa shahada ya kwanza. Hii ni hatari kubwa sana kuna ambao hata CV zetu hatuwezi kuziandika kabisa.

 

SHULE ZA MCHEPUO WA KIINGEREZA.

Kwa Tanzania kuna Shule tunazoziita English Medium primary schools. Kuna baadhi ya Watanzania wamefanikiwa kupeleka watoto wao kwenye Shule hizi. Hawa wanafundishwa kwa Lugha ya Kiingereza kuanzia darasa la Awali hadi Secondari.

Afadhali hawa hawachanganyi sana mambo na imeanza kubainika wakifika Secondary  wengi wao wanafanya vizuri ikilinganishwa na hawa ambao wamechanganya Lugha.

 

  1. #KITUGANI KINAFUNDISHWA MASHULENI? (CONTENT)

Hili nalo ni tatizo kubwa sana kwa Tanzania. Nilitarajia mimi niliyezaliwa kule BUkoba  nifundishwe namna bora ya kilimo cha ndizi  na kahawa, kulingana na mazingira yangu na namna bora ya kuzibadilisha ndizi hizo kuwa zao la biashara kwa kuziongezea thamani.

Badala yake nafundishwa Kilimo cha Mpunga Thailand au kilimo cha Matunda kule Itally. Tena kwa Lugha ya mkoloni ambayo naishia kukariri tu.

Huwa nacheka sana ninapoona mawaziri wetu wakikimbizana na Ruge mikoani kuzindua kitu kinachoitwa Fursa. Najiuliza pale Mlimani wanafundisha nini? Najiuliza pale SUA wanafundisha nini? Najiuliza shule zetu za  A Level wanafundisha nn? Huku ngazi za chini kunafundishwa nini?

Ni dhahiri sasa kinachofundishwa na ngazi tofauti tofauti za elimu Nchini content zake hazina maana kwa wahitimu na zimeshindwa kuwafanya wajiajiri. Je tunakumbuka falsafa yetu ya elimu inasemaje?

#Trend ipo hivi wanaomaliza Darasa la saba asilimia 100 wanawaza kuvuka kwenda sekondari, wanaomaliza form 4 asilimia 100 wanawaza kuvuka kwenda form six wanaomaliza form six asilimia 100 wanawaza kujiunga na vyuo vikuu.

Wakimaliza vyuo vikuu wote asilimia 100 wanawaza kwenda kuajiriwa na serikali au makampuni binafsi.

Hii ndio trend ya elimu yetu tuliyonayo kwa zaidi ya miaka 30 sasa.

 

Hatuna clear Philosophy inayotuongoza katika elimu yetu. Mwalimu Nyerere alituachia ya Education for Self reliance.

 

Katika hili Mwalimu alilenga mtu atakayehitimu hata darasa la Saba aweze kujitegemea kwa kutumia fursa zinazomzunguka.

Tatizo kubwa tulilonalo kwa sasa ni Content nyingi tunazofundisha au kufundishwa mashuleni kushindwa kutafsiri fursa tulizonazo.

 

#Shule zetu zilizokuwa zinafundisha fani mbalimbali za Ushonaji, Upishi, uashi nk tumeendelea kuziua na hata wanafunzi hawazitaki tena hizo fani.

#Ibn Khladun Mwanafalsafa wa Tunisia aliwahi kusema kuwa elimu isiwe ni ya kukaririsha watu mambo ya zamani kwa Lengo la kuwapatia vyeti.

Kwake yeye content zilizokuwa zikifundishwa zilikuwa nyingi ni za kukaririshwa na aliyeweza kukariri kwa ufasaha ndiye aliyetunukiwa cheti

Hiki ndicho tunachokiona leo katika jamii yetu, atakayeweza kukariri content za physics, Kemia, history na kadhalika huyu ndiye tuanyemgrade kuwa ana akili.

Tunampatia cheti na kumwambia songa mbele hawa ambao hawana uwezo wa kukariri, Content zetu hazijaandaliwa kuwapima uwezo wao mwingine walionao tunawagrade kuwa mmefeli na wanafeli kabisa hadi maisha. Ni kama kumpima samaki kwenye uwezo wa kukwea mti. Unamwona samaki hawezi na ni kweli hawezi lakini lipo jambo analoliweza ten sana.

#John Dewey huyu ni mwanafalsafa wa Kimarekani  yeye anatuambia tufundishe kwa kutumia Experience inayomzunguka mwanafunzi.

 

Hiki ndicho kinachofanyika kwa wenzetu wazungu, wanatemgeneza mitaala yao kulingana na kinachowazunguka ili mwanafunzi aweze kuibua fursa na vipaji alivyonavyo.

#Sisi tumeng’ang’ania kufundisha na kakaririshana colonial Rule toka 1961 hadi sasa na akili zetu zimeacha kutafsiri ni aina gani ya udongo tulionao Tanzania, tumeacha kujifunza tunawezaja kuhamisha maji pale victoria yaje Shinyanga kwenye ukame, hatuwezi kutafsiri chochote…..

Je tutaendelea kuona Boda boda ndiyo fursa pekee?

 

Je jukumu la kufundishwa content zenye tija ni la nani? Au ni mpaka tumwachie Ruge aje awaokote huko mtaani na kuja kuwafundisha Fursa?

 

#Ukiona semina za kufundishana Fursa kama hizi zikishamiri sana katika nchi fahamu kuwa Nchi haina falsafa ya Elimu na hatujui shule zina Jukumu gani.

#Mikopo yote ya kujisomesha tumewapa wale walioweza kukariri vizuri ngazi za chini, wale waliokuwa na vipaji na Talent nyingine tumewaambia waende nyumbani na hawa ndio haswa tuliopaswa kutambua tallent zao na kuzipatia mikopo ya kuziendeleza.

 

Ukiangalia Site zetu zetu kubwa kubwa makampuni yanayosimamia miradi utakuta ni wachina wanazisimamia, Juzi tulienda kuomba watu toka Uganda kuja kutafiti kama tuna mafuta nchini.

Dunia kwa sasa inawekeza katika Technolojia yaani watu wanawaza kuuza Technolojia zaidi kuliko Korosho na wanatengeneza fedha.

Technolojia hizi hatuwezi kuzivumbua kama tutafundisha Kinjekitile Ngwale kuanzia msingi hadi chuo Kikuu. Kuna haja ya kutengeneza Model mpya ya elimu yetu. Kwamba kama ni historia basi tufundishe labda darasa la ngapi tu miaka mingine inayobaki mtoto afundishwe mambo mengine yatakayomsaidia baadaye.

 

#Elimu yetu ndio chombo pekee cha kutufikisha tunakokutamani vinginevyo tutakuwa tukihangaika kila mahali kutafuta wawekezaji.

 

Hizi Reli tunazojenga na Barabara zinakuja kuwarahisihia wawekezaji wa nje kupeleka malighafi zao pale bandarini bado. Sisi tutabaki kusafirishia huko gunia mia za Korosho au Karanga. Vinginevyo tutabaki tunasubiri abiria huku njiani kuwauzia pipi, saa na headphones.

#Naamini sisi tunaozunguka na viti maofisini na kujidai wenye akili tulibarikiwa tu uwezo wa Kukariri, kuna ambao tuliwaacha mtaani walikuwa na uwezo wa kuyatafsiri mazingira kuliko sisi. Bahati yao mbaya elimu yetu haiwatambui.

#Swala la msingi la Kujiuliza tutaanza Kubadilika Lini?

 

Leave a Reply