MWASENDA DEVELOPMENT INTERVENTION (MDI - NGO)

MAWAZO YA BIASHARA (BUSINESS IDEA)

B.I 250

Habari za majukumu watanzania wenzangu;

Kwa leo napenda niwajuze kitu kimoja ambacho kikazingatiwa kinaweza kuleta mabadiliko makubwa sana ya kiuchumi  ndani ya muda mfupi kwako na kwa jamii nzima ya watanzania.

Mwasenda Development Intervention (MDI) ni shirika lisilo la kiserikali linaloendesha shughuli zake hapa nchini Tanzania; likiwa na usajili pamoja na baraka zote toka taasisi husika.

Kwa leo tunakuja na mawazo mia tano (500) ya biashara ambazo zinaweza kufanyika sehemu mbalimbali za hapa Tanzania na zinaonesha kuleta manufaa na faida kubwa kwenye jamii.

Mawazo hayo ya biashara tumeyaweka katika mafungu matatu; kilimo (agriculture), usindikaji (manufacturing)  na huduma (Services). Mawazo yote yamefanyiwa uchambuzi wa kina kuanzia namna ya kuanza, gharama za mtaji na uendeshaji na mwisho faida itakayopatikana. Kwa ujumla gharama za kunzisha biashara hizo ni kuanzia Dola za Kimarekani 500  hadi 700,000 (sawa na Tshs. 1,130,000/= hadi 1,582,000,000/=) Mawazo hayo yameandikwa kwa lugha ya Kiingereza (rahisi); hii ni kutoa mwanya kwa kila msomaji kuelewa na pia kuweza kuwashawishi wafadhili ambao lugha yao ni hiyo. MDI tunao wataalamu wanaoweza kutafisiri kwa lugha Kiswahili iwapo itatokea mhusika hajui Kiingereza.  Pesa ya mtaji wa kuanzia tunaamini watanzania walio wengi wanaweza kuipata kwa njia  mbalimbali. Njia hizo ni kama ifuatavyo:-

  1. Kupitia vikundi vya kijasiriamali
  2. Kupitia mikopo toka taasisi za kifedha
  3. Kupitia misaada toka kwa wanandugu au wafadhili wa ndani na nje ya nchi.

Walengwa wa mawazo haya ni akina nani?

  1. Vijana waliohitimu masomo (sekondari na vyuo)
  2. Wamama wa majumbani
  3. Mtu yeyote mwenye utayari wa kujiajili.

Nini kifanyike?

Wasiliana nasi; utapatiwa orodha ya mawazo ya biashara (Business Idea) pamoja na gharama za kuanzisha biashara hiyo sambamba na faida inayoweza kupatika kwa kipindi maalumu.

Ukishapitia orodha nzima utachagua ni biashara gani  unapenda kufanya na unaweza kupata mtaji wake. (suala la mtaji lisikutishe sana – utayari ndicho kitu cha msingi ni utayari wako).

MDI tunakupatia mafunzo ya muda mfupi kuhusu biashara husika. Mafunzo hayo yanaweza kuendeshwa kwa njia mbili; njia ya masafa (online coaching) au unaweza kufika kwenye vituo vyetu vya mafunzo. Utachangia gharama kidogo kwa ajili ya mafunzo;  gharama hizo zitategemeana na ukubwa wa biashara husika.

Baada ya kupata mafunzo; utapewa andiko la wazo la biashara likiwa  limechanganuliwa  kila kipengere. MDI tutaendelea kuwa washauri wako kwenye biashara hiyo.

Soma orodha hapo kwenye attachment.

Ahsanteni kwa kunielewa.

  1. I. Kahuta

Executive Secretary – MDI  Tanzania

This Post Has 2 Comments

  1. I didnt see the attachment for the 500 business ideas, i will be glad to get it

    1. Mr. Isack, angalia vyema nimeatach jamani. naweza pia kukutumia kwa e-mail yako. It seems you are serious.

Leave a Reply