MWASENDA DEVELOPMENT INTERVENTION (MDI - NGO)

MENTOR NA COMPETITOR

KUNA TOFAUTI KUBWA SANA KATI YA “MENTOR NA COMPETITOR”

#Tunapoanza kazi mpya tunatakiwa tutafute Au tutafutiwe mentors na si kutafuta au kutafutiwa Competitor.

#Kuna tofauti kati ya misamiati hiyo miwili. Mentor ni mtu unayepewa au unayemtafuta akusaidie katika kazi wakati unaanza kazi mpya au biashara mpya ambayo hujawahi kuifanya awali.

#Competitor ni mtu anayejitokeza kushindana na wewe katika field uliyopo, mara nyingi hawa hujitokeza wenyewe na hawatafutwi.

#Ni kosa kubwa kumchukua au kumfanya mtu ambaye ana skills, Uzoefu na Knowledge kubwa katika eneo la kazi yako au biashara unayofanya na kumfanya Competitor. Huyu unatakiwa umfanye mentor na si Competitor wako.

#Mark Zuckerberg CEO wa mtandao wa Facebook aliwahi kuhojiwa na Charlie Rose katika kipindi cha American talk Show, akasema nyuma ya mafanikio yake kuna Mentor anayeitwa Steve Jobs. Katika ukuraza wake wa Facebook pia Zuckerber aliwahi kumshukuru Steve Jobs kwa msaada anaompa.

#Bill Gate huyu mnamjua kutokana na utajiri wake.Aliwahi kufanyiwa mahojiano na CBC Bill Gate hakusita kumtaja mtu anayeitwa Buffet kama mtu anayemfundisha mambo ya kibiashara na namna ya kuendesha kampuni lake. Bill Gate alidai Buffet ni mtu anayemfundisha kuchukua mambo magumu na kuyafanya kuwa marahisi kabisa. Hii ni kutokana na uzoefu aliokuwa nao Buffet katika eneo jipya aliloingia Bill Gate.

#Richard Branson mwanzilishi wa kampuni la Virgin Group, aliwahi kusema kama ukiwauliza wafanyabiashara wowote waliowahi kufanikiwa wamefanikiwaje hawataacha kuwataja mentors wao. Richard Branson yeye alimtaja Freddie Laker ambaye alikuwa mfanyabiashara wa ndege kama Mentor wake.

#Hawa ni baadhi tu ya watu waliokiri kuwa Mentors wao wamewafanya kuwa kama walivyo sasa. Ni jambo la kawaida kuwa unaweza Kufanikiwa kuliko Mentor wako lakini Kamwe usimdharau au kumtupa.

TATIZO KUBWA.

#Tatizo kubwa ni watu kushindwa kutambua nani ni Mentor na ni nani Competitor wako.

#Mentor ni mtu unayetakiwa umtumie kupata maarifa na mbinu kutoka kwake. Ni senior katika eneo ulilopo liwe ni la kibiashara au ni la kiutendaji.

#Mtu ambaye ni Senior kwako katika kazi au ana maarifa zaidi yako katika eneo ulilopo ukijichanganya ukamfanya Competitor utaanguka. Mtu wa aina hiyo mtumie kama Mentor.

AINA ZA MENTOR.

#Zipo aina nyingi za mentor katika maeneo yanayotuzunguka.

1. Coach:- Huyu ni yule anayekusaidia kukupa mbinu za moja kwa moja za kupambana na tatizo. Huyu anakusikiliza anakupa mbinu halafu anakuacha unaenda kuzifanyia kazi. Mara nyingi wala watu hawezi kumjua….. wataona tu mambo yanakwenda na anakuachia upate credit wewe.

2. Star:- Tafuta mtu mwenye Career unayoitaka, kama ni kiongozi tafuta kiongozi ambaye amewahi kufanikiwa sana, chukua muda kujifunza alikuwa anafanyaje kazi.

3. Connector:- Huyu ni mtu anayekusaidia kukuunganisha na watu waliofanikiwa na wanaoweza kutoa mchango katika eneo lako. Unaweza kuwa mfanyabiashara au kiongozi lakini hujuani na watu, mtumie connector kukusaidia kukukutanisha na watu hao. Huyu atakusaidia kukutengenezea network mpya yenye mawazo tofauti.

4. Librarian:- Huyu ni yule anayekusaidia kukupa vyanzo vya maarifa. Hata kama jambo limejifichaje huyu atakusiaidia kukupa namna ya kujifunza jambo husika. Ukiwa mfanyabiashara au kiongozi huwezi kufahamu kila kitu hapa ndipo unapomhitaji mtu wa aina hii akushike mkono.

#Mwisho Si vibaya kuwa na aina zote za Mentor katika kazi unayoifanya.

Nikutakie Week-end njema (12 May 2018)

Karibu Mwasenda Development Intervention. 

 

Leave a Reply